التصنيفات
القرآن الكريم

المختصر في التفسير Kiswahili سورة [آل عمران]

۞إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰٓ ءَادَمَ وَنُوحٗا وَءَالَ إِبۡرَٰهِيمَ وَءَالَ عِمۡرَٰنَ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

السواحيلية | Kiswahili

33. Hakika Allah alimteua Adam (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake)akasujudiwa na Malaika wake, na akamteua Nuhu akamjaalia kuwa Mtume wa kwanza duniani, na kauteua ukoo wa Ibrahim akajaalia Unabii ni wenye kubakia katika kizazi chake, na kateua ukoo wa Imran, kateua wote hao pia kawatukuza juu ya watu wa zama hizo. 

ذُرِّيَّةَۢ بَعۡضُهَا مِنۢ بَعۡضٖۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

السواحيلية | Kiswahili

34. Hao waliotajwa miongoni mwa Manabii na vizazi vyao vyenye kufuata njia yao Ni wazao wao kwa wao katika kumpwekesha Allah na kufanya matendo mema, wanarithishana tabia njema, na Allah ni Mwenye kusikia maneno ya waja wake, na Mwenye kujua vitendo vyao; kwa sababu hiyo huchagua awatakao miongoni mwao, na huteua awatakao. 

إِذۡ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ عِمۡرَٰنَ رَبِّ إِنِّي نَذَرۡتُ لَكَ مَا فِي بَطۡنِي مُحَرَّرٗا فَتَقَبَّلۡ مِنِّيٓۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

السواحيلية | Kiswahili

35. Kumbuka -Ewe Mtume- Alipo sema mke wa Imran Mama yake Maryam (Rehma na amani za Allah ziwe juu yake): Mola wangu Mlezi! Nimejiwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu kwa ajili yako, akutumikie na kuitumikia nyumba yako, basi nikubalie hilo, Hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia maombi yangu, Mwenye kujua nia yangu. 

فَلَمَّا وَضَعَتۡهَا قَالَتۡ رَبِّ إِنِّي وَضَعۡتُهَآ أُنثَىٰ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا وَضَعَتۡ وَلَيۡسَ ٱلذَّكَرُ كَٱلۡأُنثَىٰۖ وَإِنِّيسَمَّيۡتُهَا مَرۡيَمَ وَإِنِّيٓ أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ

السواحيلية | Kiswahili

36. Basi ulipo kamilika ujauzito alijifungua akisema kwa kutoa udhuru- alikuwa anataraji kuwa ni Mtoto wa kiume-: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke, na Allah anajua sana niliye mzaa, Na mwanamume aliye kuwa anataraji si sawa na mwanamke aliyo pewa kwa nguvu na maumbile. Na mimi nimemwita Maryamu, Nami namkinga kwako yeye na uzao wake kutokana na Shetani aliye fukuzwa katika Rehma zako. 

فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٖ وَأَنۢبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنٗا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّاۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيۡهَا زَكَرِيَّا ٱلۡمِحۡرَابَ وَجَدَعِندَهَا رِزۡقٗاۖ قَالَ يَٰمَرۡيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَٰذَاۖ قَالَتۡ هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٍ

السواحيلية | Kiswahili

37. Tena Mola wake Mlezi akampokelea nadhiri yake kwa mapokeo mema, na akamkuza makuzo mema, wakamfanyia upole waja wema, na akamfanya Zakariya (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake) awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake sehemu ya Ibada alimkuta na vyakula safi, Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akamjibu: Hivi vinatoka kwa Allah, na Allah humruzuku amtakaye rizki kubwa bila ya hesabu. 

وَإِذۡ قَالَتِ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَٰمَرۡيَمُ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصۡطَفَىٰكِ وَطَهَّرَكِ وَٱصۡطَفَىٰكِ عَلَىٰ نِسَآءِ ٱلۡعَٰلَمِينَ

السواحيلية | Kiswahili

42. Na kumbuka -Ewe Mtume- pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu (Rehma na amani za Allah ziwe juu yake): Kwa hakika Allah amekuteua kutokana na sifa nzuri ulizonazo, na akakutakasa kutokana na upungufu, na akakutukuza kuliko wanawake wote wa zama zako. 

يَٰمَرۡيَمُ ٱقۡنُتِي لِرَبِّكِ وَٱسۡجُدِي وَٱرۡكَعِي مَعَ ٱلرَّـٰكِعِينَ

السواحيلية | Kiswahili

43. Ewe Maryamu, zidisha kisimamo katika Swala zako, na usujudu kwa ajili ya Mola wako, na urukuu pamoja na wenye kurukuu miongoni mwa waja wake wema. 

ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهِ إِلَيۡكَۚ وَمَا كُنتَ لَدَيۡهِمۡ إِذۡ يُلۡقُونَ أَقۡلَٰمَهُمۡ أَيُّهُمۡ يَكۡفُلُ مَرۡيَمَ وَمَا كُنتَلَدَيۡهِمۡ إِذۡ يَخۡتَصِمُونَ

السواحيلية | Kiswahili

44. Habari zote hizo ni za Zakariya na Maryamu (Rehma na amani za Allah ziwe juu yao) ni khabari za ghaibu tunazo kufunulia -Ewe Mtume- nawe hukuwa nao walipo wanazuoni wao na wema wao wakizozana nani kati yao anayo haki ya kumlea Maryamu, hadi wakapiga kura wakatupa kalamu zao, ikafaulu kalamu ya Zakariya (Rehma na amani za Allah ziwe juu yake)

إِذۡ قَالَتِ ٱلۡمَلَـٰٓئِكَةُ يَٰمَرۡيَمُ إِنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٖ مِّنۡهُ ٱسۡمُهُ ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ وَجِيهٗا فِيٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ

السواحيلية | Kiswahili

45. Na kumbuka -Ewe Mtume- pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Allah anakubashiria mtoto atakaye zaliwa bila ya baba, itakuwa kwa neno litokalo kwa Allah kwa kusema: Kuwa ikawa mtoto kwa idhini ya Allah, Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibu na Allah. 

وَيُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗا وَمِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

السواحيلية | Kiswahili

46. Naye atazungumza na watu katika utoto wake kabla muda wa kuongea haujafikia, na ataongea nao katika utuuzima wake, atawaambia mambo yaliyo na kheri katika dunia yao na akhera yao, na atakuwa katika watu wema kwa maneno yao na mambo yao. 

قَالَتۡ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٞ وَلَمۡ يَمۡسَسۡنِي بَشَرٞۖ قَالَ كَذَٰلِكِ ٱللَّهُ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۚ إِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَايَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

السواحيلية | Kiswahili

47. Maryamu akasema kwa mshangao vipi atakuwa na mtoto bila ya mume: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu si kwa halali wala kwa haramu?! Malaika akasema kumwambia: Ndivyo vivyo hivyo, mfano wa Allah kukuumbia mtoto bila ya baba, huumba apendacho kwa njia isiyo ya kawaida, Anapo hukumu jambo huliambia: Kuwa! Likawa, hashindwi na chochote.

وَيُعَلِّمُهُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ

السواحيلية | Kiswahili

48. Na atamfunza kuandika na kupatia na kumuafikisha katika kauli na matendo, na atamfundisha Taurati aliyo iteremsha kwa Mussa (Rehma na amani za Allah ziwe juu yake), na Injili ambayo atamteremshia.