التصنيفات
القرآن الكريم

المختصر في التفسير Kiswahili سورة [النساء]

وَبِكُفۡرِهِمۡ وَقَوۡلِهِمۡ عَلَىٰ مَرۡيَمَ بُهۡتَٰنًا عَظِيمٗا

السواحيلية | Kiswahili

156. Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-, uongo mkubwa wa zinaa Tuliwalaani. 

يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا تَغۡلُواْ فِي دِينِكُمۡ وَلَا تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ إِنَّمَا ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ رَسُولُٱللَّهِ وَكَلِمَتُهُۥٓ أَلۡقَىٰهَآ إِلَىٰ مَرۡيَمَ وَرُوحٞ مِّنۡهُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۖ وَلَا تَقُولُواْ ثَلَٰثَةٌۚ ٱنتَهُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ إِنَّمَاٱللَّهُ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ سُبۡحَٰنَهُۥٓ أَن يَكُونَ لَهُۥ وَلَدٞۘ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلٗا

السواحيلية | Kiswahili

171. Sema -Ewe Mtume- kuwaambia Manaswara waliopewa Injili: Msichupe mipaka katika Dini yenu, wala msiseme juu ya Allah kuhusu mambo ya Issa -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake- ila kwa lililo kweli, Hakika Masihi Issa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Allah amemtuma kwa haki, amemuumba kwa neno lake alilomtuma Jibril -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake- kwa Maryamu, nalo ni kauli yake: Kuwa ikawa nayo ni roho iliyotoka kwa Allah kaipuliza Jibril kwa amri ya Allah, Basi Muaminini Allah na Mitume wake wote bila ya kubaguwa baina yao, Wala msiseme: Uungu utatu, Komeni na kauli hiyo ya uongo mbaya kuacha kwenu itakuwa kheri kwenu duniani na akhera, Hakika Allah ni Allah mmoja tu Ametukuka na kutokuwa na mshirika na mtoto, Yeye kajitosheleza, Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi na vilivyopo baina yake, Na Allah anatosha kuwa Msimamizi wa vilivyomo mbinguni na ardhini na muendeshaji wake.