التصنيفات
القرآن الكريم

المختصر في التفسير Kiswahili سورة [المائدة]

لَّقَدۡ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَۚ قُلۡ فَمَن يَمۡلِكُ مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـًٔا إِنۡ أَرَادَ أَن يُهۡلِكَٱلۡمَسِيحَ ٱبۡنَ مَرۡيَمَ وَأُمَّهُۥ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗاۗ وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَاۚ يَخۡلُقُ مَايَشَآءُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

السواحيلية | Kiswahili

17. Hakika wamekufuru miongoni mwa Manaswara waliosema: Allah ni Masihi Issa mwana wa Maryamu, Sema uwaambie hao -Ewe Mtume-: Ni nani mwenye kumiliki chochote mbele ya Allah ikiwa Yeye angetaka kumuangamiza Masihi Issa mwana wa Maryamu, na mama yake, na kuwaangamiza wote waliomo katika ardhi akitaka kuwaangamiza?! Na ikiwa hakuna yeyote awezae kuzuia hilo yaonyesha ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki zaidi ya Allah, na kwamba wote: Issa mwana wa Maryamu na mama yake na viumbe wote wameumbwa na Allah, mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ni vya Allah Huumba apendavyo, Na alivyo taka kamuumba Issa -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-; Yeye ni mja wake na Mtume wake, Na Allah anao uwezo juu ya kila kitu.

مَّا ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَ إِلَّا رَسُولٞ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهِ ٱلرُّسُلُ وَأُمُّهُۥ صِدِّيقَةٞۖ كَانَا يَأۡكُلَانِ ٱلطَّعَامَۗ ٱنظُرۡكَيۡفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ ٱنظُرۡ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ

السواحيلية | Kiswahili

75. Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume wa Allah kati ya Mitume, anafikiwa na umauti kama wanavyo fikiwa, Na mama yake Maryamu -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-, ni mwingi wa ukweli na kusadikisha, Wote wawili walikuwa wakila chakula kwa kukihitajia, vipi watakuwa waungu wawili huku wanahitajia chakula?! Angalia -Ewe Mtume- kwa kuzingatia: jinsi tunavyo wabainishia Aya zinazo onyesha upweke wetu, na juu ya ubatilifu walionao katika kuchupa kwao mipaka juu ya kunasibisha Uungu kwa asiyekuwa Allah, pamoja na yote hayo wanakanusha Aya hizi, kisha angalia kwa kuzingatia: vipi wanavyo geuza haki na hizi Aya zilizo wazi zinazo onyesha juu ya upweke wa Allah. 

إِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ٱذۡكُرۡ نِعۡمَتِي عَلَيۡكَ وَعَلَىٰ وَٰلِدَتِكَ إِذۡ أَيَّدتُّكَ بِرُوحِ ٱلۡقُدُسِ تُكَلِّمُ ٱلنَّاسَفِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗاۖ وَإِذۡ عَلَّمۡتُكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَۖ وَإِذۡ تَخۡلُقُ مِنَ ٱلطِّينِ كَهَيۡـَٔةِ ٱلطَّيۡرِبِإِذۡنِي فَتَنفُخُ فِيهَا فَتَكُونُ طَيۡرَۢا بِإِذۡنِيۖ وَتُبۡرِئُ ٱلۡأَكۡمَهَ وَٱلۡأَبۡرَصَ بِإِذۡنِيۖ وَإِذۡ تُخۡرِجُ ٱلۡمَوۡتَىٰ بِإِذۡنِيۖ وَإِذۡكَفَفۡتُ بَنِيٓ إِسۡرَـٰٓءِيلَ عَنكَ إِذۡ جِئۡتَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

السواحيلية | Kiswahili

110. Na kumbuka pale Allah alipo sema kumwambia Issa -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-: Ewe Issa bin Maryamu, Kumbuka neema yangu juu yako nilipo kuumba bila ya baba, na kumbuka neema yangu juu ya mama yako Maryamu -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-, nilipo mteua kuliko wanawake wote wa zama zake, na kumbuka neema nilizo kuneemesha juu yako nilipo kutia nguvu kwa Jibril -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-, ukazungumza na watu -na wewe ukiwa mtoto wa kunyonya- kwa kuwalingania kwa Allah, na unaongea nao ukiwa katika utuuzima uliyo tumwa nayo kwao, Na katika neema niliyo kuneemesha kukufunza kuandika, na nilikufundisha Taurati niliyo iteremsha kwa Mussa -Rehma na amani za Allah ziwe juu yake-, na Injili niliyo kuteremshia, Na nilikufundisha undani wa sheria na faida zake na hekma zake, na katika niliyo kuneemesha unatengeneza udongo kwa sura ya ndege, kisha unapuliza ikawa ndege, na unamponya aliye zaliwa kipofu, na unamponya mwenye ukoma, anakuwa na ngozi nzuri, na unawafufua wafu kwa kumuomba Allah awahuishe, yote hayo kwa idhini yangu, na katika niliyo kuneemesha ni kukuondolea Wana wa Israili walipo kusudia kukuua ulipo wajia na miujiza ya wazi, hawakuwa na lao zaidi ya kukupinga, na wakasema: Haya aliyo kuja nayo Issa si lolote ila ni uchawi mtupu.

وَإِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ءَأَنتَ قُلۡتَ لِلنَّاسِ ٱتَّخِذُونِي وَأُمِّيَ إِلَٰهَيۡنِ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالَ سُبۡحَٰنَكَمَا يَكُونُ لِيٓ أَنۡ أَقُولَ مَا لَيۡسَ لِي بِحَقٍّۚ إِن كُنتُ قُلۡتُهُۥ فَقَدۡ عَلِمۡتَهُۥۚ تَعۡلَمُ مَا فِي نَفۡسِي وَلَآ أَعۡلَمُ مَا فِينَفۡسِكَۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّـٰمُ ٱلۡغُيُوبِ

السواحيلية | Kiswahili

116. Na kumbuka pale Allah atakapo sema siku ya Qiyama kumwambia Issa bin Maryam -Rehma na amani za Allah ziwe juu yao-: Ewe Issa bin Maryam, Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu waabudiwa wawili badala ya Allah? Na Issa akajibu kwa kumtakasa Mola wake: Hainipasi mimi kuwaambia kinyume na haki, Na tujaalie kama nimesema hayo bila ya shaka umekwisha yajua kwa sababu halijifichi jambo kwako, Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako, Hakika Wewe peke yako ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana na yaliyo dhahiri.