التصنيفات
القرآن الكريم

المختصر في التفسير Kiswahili سورة [مريم]

وَٱذۡكُرۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَرۡيَمَ إِذِ ٱنتَبَذَتۡ مِنۡ أَهۡلِهَا مَكَانٗا شَرۡقِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

16. Na kumbuka -Ewe Mtume- katika Quran hii iliyo shushwa juu yako kuhusu khabari za Maryamu (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), pale alipo jitenga na jamaa zake akawa peke yake upande wa mashariki. 

فَٱتَّخَذَتۡ مِن دُونِهِمۡ حِجَابٗا فَأَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرٗا سَوِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

17. Na akajiwekea pazia kujikinga nao ili wasimuone anapokuwa akifanya Ibada ya Mola mlezi wake, Tukampelekea Jibril (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), akajifananisha kwake kwa sura ya binaadamu alie kamilika maumbile, akaogopa ya kwamba anataka kumfanyia kitu kibaya. 

قَالَتۡ إِنِّيٓ أَعُوذُ بِٱلرَّحۡمَٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

18. Alipo muona katika umbile la binaadamu aliye kamilika maumbile akimuelekea akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehma aniepushe nawe kunifanyia kibaya, ukiwa Wewe ni mwenye kumuogopa Allah. 

قَالَ إِنَّمَآ أَنَا۠ رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَٰمٗا زَكِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

19. Jibril (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake)akasema: Mimi sio binaadamu, Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola mlezi wako kanituma kwako ili nikupatie zawadi ya mtoto mzuri aliye takasika. 

قَالَتۡ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَٰمٞ وَلَمۡ يَمۡسَسۡنِي بَشَرٞ وَلَمۡ أَكُ بَغِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

20. Akasema Maryamu kwa mshangao: Nitampataje mtoto hali mwanaadamu yeyote hajanigusa wala yeyote hajanikaribia, wala mimi sio mzinifu hadi ifikie kupata mtoto?! 

قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٞۖ وَلِنَجۡعَلَهُۥٓ ءَايَةٗ لِّلنَّاسِ وَرَحۡمَةٗ مِّنَّاۚ وَكَانَ أَمۡرٗا مَّقۡضِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

21. Jibril akasema kumwambia: Mambo ni kama usemavyo ya kwamba hujaguswa na mume wala yeyote wala sio mzinifu, lakini Mola mlezi wako amesema: Hayo ya kumuumba mtoto bila ya baba ni vyepesi kwangu, Na ili awe mtoto tulio kuzawadia kuwa ni Alama kwa watu juu ya uwezo wa Allah, na Rehma itokayo kwetu kwako na atakaye muamini, na hilo la kuumbwa mtoto wako ni jambo lilio kwisha hukumiwa kutoka kwa Allah, limekwisha andikwa kwenye ubao wa kuhifadhia. 

۞فَحَمَلَتۡهُ فَٱنتَبَذَتۡ بِهِۦ مَكَانٗا قَصِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

22. Basi akabeba mimba yake baada ya Malaika kupuliza, na akaondoka nayo mpaka sehemu iliyo mbali na watu. 

فَأَجَآءَهَا ٱلۡمَخَاضُ إِلَىٰ جِذۡعِ ٱلنَّخۡلَةِ قَالَتۡ يَٰلَيۡتَنِي مِتُّ قَبۡلَ هَٰذَا وَكُنتُ نَسۡيٗا مَّنسِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

23. Akafikwa na machungu, akajielekeza kwenye shina la mtende, akasema Maryamu (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake): Laiti ningeli kufa kabla ya siku hii, na nikawa kitu kisicho tajwa ili nisidhaniwe vibaya. 

فَنَادَىٰهَا مِن تَحۡتِهَآ أَلَّا تَحۡزَنِي قَدۡ جَعَلَ رَبُّكِ تَحۡتَكِ سَرِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

24. Akamwita Issa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola mlezi wako amejaalia chini yako kijimto kidogo cha maji utakunywa. 

وَهُزِّيٓ إِلَيۡكِ بِجِذۡعِ ٱلنَّخۡلَةِ تُسَٰقِطۡ عَلَيۡكِ رُطَبٗا جَنِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

25. Na kamata hilo gogo la mtende litikise utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu muda huo.

فَكُلِي وَٱشۡرَبِي وَقَرِّي عَيۡنٗاۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ ٱلۡبَشَرِ أَحَدٗا فَقُولِيٓ إِنِّي نَذَرۡتُ لِلرَّحۡمَٰنِ صَوۡمٗا فَلَنۡ أُكَلِّمَٱلۡيَوۡمَ إِنسِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

26. Basi kula tende mbivu, na kunywa maji, na itulizane nafsi yako kwa kujifungua na wala usihuzunike, Na pindi ukimuona mtu yeyote akakuuliza kuhusu khabari za kujifungua basi mwambie: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Allah ya kufunga kwa kuto zungumza, hivyo leo sitasema na mtu yeyote. 

فَأَتَتۡ بِهِۦ قَوۡمَهَا تَحۡمِلُهُۥۖ قَالُواْ يَٰمَرۡيَمُ لَقَدۡ جِئۡتِ شَيۡـٔٗا فَرِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

27. Maryamu akenda na mwanaye kwa jamaa watu wake huku amembeba, Wakasema watu wake kwa kukanusha: Ewe Maryamu! Hakika umeleta na kuzua kitu kikubwa, unakuja na mtoto bila ya baba. 

يَـٰٓأُخۡتَ هَٰرُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ ٱمۡرَأَ سَوۡءٖ وَمَا كَانَتۡ أُمُّكِ بَغِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

28. Ewe unaye fanana na Harun kwa Ibada (naye ni mtu mwema) Baba yako hakuwa mtu mzinifu, wala mama yako hakuwa kahaba, Wewe ni katika nyumba takatifu inayo julikana kwa wema, inakuwaje waleta mtoto asiyekuwa na baba?! 

فَأَشَارَتۡ إِلَيۡهِۖ قَالُواْ كَيۡفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي ٱلۡمَهۡدِ صَبِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

29. Akawaashiria kwa mtoto wake Issa (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake)akiwa amebebwa, Wakasema watu wake kwa kustaajabu: Vipi tumsemeshe aliye mdogo naye kabebwa?! 

قَالَ إِنِّي عَبۡدُ ٱللَّهِ ءَاتَىٰنِيَ ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلَنِي نَبِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

30. Akasema Issa (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake): Mimi ni mja wa Allah, amenipatia Injili, na kanijaalia kuwa Nabii miongoni mwa Manabii wake. 

وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيۡنَ مَا كُنتُ وَأَوۡصَٰنِي بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ مَا دُمۡتُ حَيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

31. Na amenijaalia ni mwenye kuwasaidia waja popote pale niwapo, Na ameniusia kutekeleza Swala na kutoa Zaka muda wote wa uhai wangu. 

وَبَرَّۢا بِوَٰلِدَتِي وَلَمۡ يَجۡعَلۡنِي جَبَّارٗا شَقِيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

32. Na kanijaalia nimtendee wema mama yangu, Wala hakunifanya niwe jeuri katika kumtii Mola mlezi wangu, wala mwenye kumuasi. 

وَٱلسَّلَٰمُ عَلَيَّ يَوۡمَ وُلِدتُّ وَيَوۡمَ أَمُوتُ وَيَوۡمَ أُبۡعَثُ حَيّٗا

السواحيلية | Kiswahili

33. Na mwenye amani kutokana na Shaitwani na wasaidizi wake juu yangu siku niliyo zaliwa na siku nitakayo kufa na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai siku ya Qiyama, hakunichezea Shaitwani sehemu hizo tatu zinazo tisha. 

ذَٰلِكَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَۖ قَوۡلَ ٱلۡحَقِّ ٱلَّذِي فِيهِ يَمۡتَرُونَ

السواحيلية | Kiswahili

34. Huyo mwenye sifa hizo ndiye Issa mwana wa Maryamu, na hayo maneno ndiyo kauli ya haki, sio kama wanavyo sema walio potea ambayo wanashaka kwa hilo na kutofautiana. 

مَا كَانَ لِلَّهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٖۖ سُبۡحَٰنَهُۥٓۚ إِذَا قَضَىٰٓ أَمۡرٗا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

السواحيلية | Kiswahili

35. Haifai kwa Allah kuwa na mtoto, Yeye ametakasika kwa hilo, na Anapo lihukumu jambo basi yatosha kwake kuliambia tu: (Kuwa) Likawa bila ujanja, Mwenye kuwa hivyo ni mwenye kutakasika na kuwa na mtoto.