التصنيفات
القرآن الكريم

المختصر في التفسير Kiswahili سورة [الأنبياء]

وَٱلَّتِيٓ أَحۡصَنَتۡ فَرۡجَهَا فَنَفَخۡنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلۡنَٰهَا وَٱبۡنَهَآ ءَايَةٗ لِّلۡعَٰلَمِينَ

السواحيلية | Kiswahili

91. Na kumbuka -Ewe Mtume- kisa cha Maryamu (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), aliye linda utupu wake kutokana na zina, Allah akamtumia Malaika Jibril (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), akampulizia roho akambeba Issa (Rehma na Amani za Allah ziwe juu yake), na akawa yeye na mtoto wake Issa kuwa ni Ishara kwa watu kutokana na uwezo wa Allah, na kwamba Yeye hashindwi na chochote pale alipo muumba bila ya baba.